Timu ya taifa ya tanzanzia , Taifa stars, usiku huu imefanikiwa kuchukua nafasi ya mshindi wa tatu katika michuano ya COSAFA huko bondeni kwa mzee madiba.
Kikosi hicho kinachoongozwa na kocha Salumu Mayanga kimeonesha uwezo mkubwa katika michuano hio ya nchi za ukanda wa afrika kusini.
Taifa stars imefanikiwa kushinda kwa mikwaju ya penati dhidi ya lesotho 4-3
Penati za Tanzania zilipigwa na Shiza kichuya, Himid Mao mkami,Simon Msuva, Raphael Daudi, Abdi Banda. Kwa upande wa tanzania shiza kichuya alikosa mkwaju wa penati ambao ndo ulikua wa kwanza lakini vijana hao hawakukata tamaa na kupiga zingine na kutia kambani zote zilizofatia. Pia kiwango cha juu kwa golikipa wa taifa stars SAID MOHAMED "NDUDA" kwa kuokoa mkwaju mmoja na kufanikiwa kuipa stars ushindi katika mchezo huo dhidi ya lesotho
Tanzaniaaaa oyeeeeee!!!!!!!!!
BY:MC. RUGAMBWA
Maoni