TAIFA STARS YAPANDA KATIKA VIWANGO VYA FIFA.

Shirikisho la soka duniani limetoa viwango vipya vya timu, na timu ya Tanzania imefanikiwa kupanda nafasi 25 na kutua katika nafasi ya 114.



kikosi cha taifa stars.

FIFA wametumia michuano ya COSAFA kupanga viwango hivyo na kitendo cha taifa stars kufanya vizuri katika michuano hio kumeisaidia kupandisha timu hio nafasi 25 katika viwango vya fifa duniani. Taifa stars bado iko nchini afrika kusini kusubiria mchezo wao wa mshindi wa tatu wakikutana na lesotho siku ya tarehe 7/7/2017.  Na baada  ya hapo itakua ikijiandaa kuchuana na  timu ya taifa ya Rwanda AMAVUBI [ambayo inashika nafasi ya 127 duniani]  ili kutafuta nafasi ya kushiriki katika michuano ya CHAN ambayo ni kombe la maitaifa afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani ya afrika.




kocha wa taifa stars SALUM MAYANGA.




                                                                                                       BY; MC.RUGAMBWA

Maoni