NGASA APANGA KUFANYA MAAFA

Mshambuliaji  Mrisho khalfan Ngassa msimu huu haukuwa mzury kwake akiitumikia timu ya mbeya city. Ngasa aliuzwa katika klabu ya free state ya afrika kusini na akacheza nusu msimu na baadae kuamua kuvunja mkataba na kwenda katika klabu ya fanja ya oman . Alivyokua huko ngasa hakudumu na akaamua kurudi nyumbani na kusajili katika klabu ya mbeya city wakati wa dirisha dogo  mwezi december.



MRISHO NGASA akisaini mkataba na mbeya city mwezi december.


Lengo la ngassa kusaini mkataba na timu ya nyumbani ni kujifua upya ili kuweza kupata nafasi nyingine ya kusajiliwa na klabu kubwa hapa nchini hasa klabu yake kipenzi DAR YOUNG AFRICAN,  ngassa alishindwa kufanya hivyo baada ya kiwango chake kuwa chini msimu huu tofauti na zamani alivyokuwa.

Sasa ivi Mrisho yupo mwanza akijifua akitaka kuthibitisha wanafamilia ya soka nchini Tanzania kwamba yeye bado hajaisha na anajipanga kufanya maafa katika ligi kuu bara msimu wa 2017/2018



Mrisho khalfan Ngassa akiwa katika uzi wa mbeya city msimu wa 16/17



                                                                                                                 BY; MC.RUGAMBWA.
                                                                                                                        

Maoni