BRADLEY, DEFOE NA SOKA

Ni leo tarehe 7/72017 ambapo familia ya soka duniani imepata msiba mzitoo wa kijana mdogo mpenzi wa mpira wa miguuu na shabiki mkubwa wa klabu ya sunderland BRADLEY LOWERY. Ni taarifa ya kusikitisha sana kwa wanafamilia ya soka hasa wale mashabiki wa timu ya sunderland ya ligi kuu england.

Kwa msiba huu ,mjini wanasema kwamba ni mtoto wa juzi tuuh, kwa maana kijana huyo alizaliwa mwaka 2011 na kuaga dunia miaka sita baadae, inasikitisha sana. Bradley aliupenda sana mpira wa soka, aliipenda sana sunderland na mtu aliyekuwa akimpa raha sana mpirani ni mshambuliaji wa sunderland Jermain Defoe. Kijana huyo alipenda sana soka na alikua mfano bora sana kwa mashabiki wa mpira wa miguu kwa ujumla.
Bradley ni kati ya watu wapambanaji maana afya ya mwili wake ilipambana sana na ugonjwa uliokuwa unamsumbua ambao ni cancer. Cancer ni ugonjwa ambao mara nyingi watu wakiupata hawadumu sana hapa duniani. Aliteseka sana na cancer ila hakuacha kuupenda mpira wa miguu, hakuacha kuishabikia sunderland na hata sunderland ilivyokuwa haifanyi vizury ila kijana huyo hajawah kukata tamaa kuishabikia timu hiyo hata alipokuwa kitandani pale hospitali.
Yote ni ya mungu na kila nafsi itaonja mauti, dunia nzima roho zetu zipo pale mitaa ya stadium of light nchini uingereza kuomboleza msiba wa kijana huyu wa soka. Bwana ametoa na bwana akatwaa jina lake liimidiwe
Bradley lowery 2011-2017
"Inna lillah wainalillah rajiun"
                                   BY:MC RUGAMBWA.

Maoni