Beki wa kati na mwenye kimo kirefu wa simba sc. Abdi Banda akamilisha usajili wake na timu mpya huko afrika kusini. Beki huyo aliyeichezea simba kwa kipindi cha miaka miwili akitokea klabu ya coastal union ya tanga kafanikiwa kufunga ndoa ya miaka mitatu na klabu inayoshiriki ligi kuu afrika kusini BAROKA FC.
Banda aliaga kabla hata ya fainalai ya kombe la FA, na kusema kuwa anaenda kutafuta maisha mapya ya soka la kulipwa huko nje. Mchezaji huyo alipata nafasi ya kufanya majaribio kipindi kile aliposimamishwa kwenye ligi kwa ajili ya utovu wa nidhamu. Banda alifanya majaribio na kufuzu na aliporudi alikataa kuongeza mkataba na klabu ya simba kwa sababu alikua ana uhakika wa dili hilo la kucheza soka la kulipwa kukamilika.
Banda anafungua njia kwa wachezaji wengine wa tanzania na pia wachezaji haswa wenye umri mdogo wasibweteke waendelee kupambana ili kutimiza malengo yao
Kila la heri Abdi Banda , ipeperushe vyema bendera ya Tanzania
Maoni