BALE ATEMA CHECHE KALI MADRID

Wakala wa mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Walesi Gareth Bale bwana Jonathan Barnett amesema lazima mazungumzo makubwa baina ya mchezaji na klabu yawepo kabda ya mwanzo wa msimu mpya.


"Nafikiri tunabidi tuwe na mazungumzo makubwa baina yetu na klabu ya Real Madrid tuone tunaelekea wapi"

"Anaitaji msimu mzuri ukilinganisha na msimu uliopita ,anataka kucheza sana nafikiri ni kati ya Wachezaji watatu au wanne bora duniani" aliongezea 

"kwa mtu kama yeye ana hitaji kucheza,si pesa"


"Anataka kushinda Ballorn d'or ,nafikiri anaweza , nafikiri ni mchezaji bora wa Uingereza ambaye anacheza soka nje ya Uingereza, na goli katika ligi ya mabigwa ulaya nafikiri alijionesha ni bora katika mechi kubwa za dunia"

"Anatakiwa kucheza mpira, nahitaji acheze katika timu yangu,lakini ana nafasi nyingi pia "

Habari na  Prosper Bartholomew.


Maoni