Zinedine Zidane ni kocha wa muispaniola Marco Ansensio haikuwa hiyo tu kusubiria kuwa kocha , staa huyo pia alifichua alikuwa amebandika picha ya mshambuliaji huyo wa zamani wa Ufaransa chumbani mwake.
Akiwa tayari ashaanza kuandaa mazingira mema dimbani Santiago Bernabeu wakati mashabiki wanamtaja kila kona staa huyu mdogo mhispaniola.
Marco Ansensio anafanya kazi yake chini ya role model wake Zidane ambaye ni kocha wake na amekuwa akimpa nafasi ya kuonesha kipaji chake .
"Nilikuwa na picha yake ukutani mwa chumbani mwangu na alikuwa role model wangu nilipokuwa mdogo"
"Alikuwa na kipaji alifanya kila nikipendacho alipokuwa uwanjani "
Ansensio pia ana imani Real Madrid wanaweza kunyakua taji la ligi ya mabigwa Ulaya kwa mara ya tatu mfululizo
"katika ligi ya mabigwa Ulaya dhidi ya PSG nafikiri tuliwaonesha watu kuwa sisi bado ni bora kama tu mwaka uliopita (msimu uliopita) , na tunaweza kufikia kitu tena napo msimu huu"
"Nafikiri sjabadilika ninavyocheza bali nmekuwa nikiamini katika mchezo ninaocheza"
"Sitaki na sijawai fikiria vitu vingi,nataka vitu viteremke na vije vyenyewe hapo ndo nafurahi na kusikia raha"
Licha ya ligi ya mabigwa Ulaya ni kuhusu kombe la dunia linalofanyika katika majira ya kiangazi baadaye mwaka huu nchini Urusi alisema,
"Sisi Hispania , tuna wachezaji wazuri wanaocheza vizuri ndani ya kocha mzuri (Lopertegui),nafikiri tunaweza fika mbali"
Makala na Prosper Bartholomew.
simu:+255716243875.
Barua pepe: barthaprosper@gmail.com.
Maoni