LIVERPOOL YAWACHAFUA MAN CITY NDANI NA NJE YA UWANJA

Kabda ya mchezo wa ligi ya mabigwa Ulaya kati ya Liverpool dhidi ya Manchester city dimbani Anfield mashabiki wa Liverpool walichukua uamuzi wa kurusha na kurushia makopo katika gari la wachezaji wa klabu ya Manchester city.

Na kurusha moshi mwekundu katika taarifa iliyotoka vioo vya gari na uharibifu kidogo umetokea na Manchester city walifanya mikakati ya basi la kuwasafirisha baada ya mchezo huo wa kufa na kupona uliofanyika dimbani Anfield .

Kocha wa Manchester city aliiambia BT sport kuwa wamekubwa na butwaa ukilinganisha na kilichowasibu Dortmund msimu uliopita.

Shirikisho la soka  la UEFA lilisema litachunguza mara moja utovu huo wa nidhamu uliofanywa na kuwaweka raia wema na askari katika hali ya hatarishi ya maisha katika kupambana na hali hiyo.

Kwa upande wa Klopp kocha wa Liverpool aliomba msamaa kwa niaba ya klabu akisema nao wamesikitishwa na kitendo hicho.

Kwa upande wa uwanjani klabu ya Liverpool wamewachafua klabu ya City kwa mabao matatu kwa bila huku Salah akifunga goli lake la 38 katika mashindano yote kabda hajapata jeraha lililomtoa nje na nafasi yake kuchukuliwa na Wijnladium huku Chermberlain na Mane wakifunga pia. Henderson nae amefungiwa kucheza mchezo wa raundi ya pili kwa kadi ya njano alioneshwa usiku wa leo ,Manchester city walishidwa kupiga shuti lilolenga goli wakifanya hivyo kwa mara ya kwanza tangu 2016 Octoba dhidi ya Manchester united.

Habari na Prosper Bartholomew.
simu:+255716243875.
barua pepe: barthaprosper@gmail.com.

Maoni