CHELSEA KUUMIZWA KICHWA NA WAFUNGAJI WAKE

Klabu ya Chelsea inayoshiriki ligi kuu Uingereza ina wafungaji 4 wa kiwango cha kati wawili wako ndani ya klabu wengine wanapandisha kiwango katika timu mbalimbali Ulaya kwanza Michy Batshuayi aliyeko Dortmund na Tammy Abraham anayeitumikia Swansea city na walioko Chelsea ni Olivier Girood na Alvaro Morata .


Alvaro Morata tengia atue klabuni Chelsea amefunga mabao 12 msimu huu katika mashindano yote na fomu yake imekuwa ya kushuka na kupanda kwa namna nyingine si katika fomu waliotarajia mabosi wake wa Chelsea.

Olivier Girood ametua klabuni Chelsea januari hii ata hivyo bado ajafunga katika michezo mieili aliyotumikia klabu hiyo ameishia kutoa pasi ya bao moja .


Michy Batshuayi ametua kwa mkopo klabuni Dortmund na ameshawafungia mabao 5 katika mechi 3 tu na akiwa Chelsea msimu huu akifunga mabao 10 katika mashindano yite.

Tammy Abraham yuko klabuni Swansea city kwa mkopo wake wa msimu mzima na amefunga mabao zaidi ya 6 katika klabu hiyo inayo haha haha kutoshuka daraja .

Chelsea bado wana vijana watakao graduate kutoka academi ambao wanafanya bora sasa Chelsea chini ya Muitaliano  Antonio Conte atabidi kuchagua vijana wawili atakao baki nao msimu wa 2018-19.

Makala na Prosper Bartholomew
Baruapepe barthaprosper@gmail.com

Maoni