TUZO ZA BBC: KIJANA WA CITY APATA TUZO , WAZAZI WA BRADLEY WAPEWA TUZO BADALA YAKE , HARRY KANE KATOKA MO FARAH KAPATA:
Kiungo mwenye miaka 17 Phil Foden anayeichezea Manchester city ametunikiwa tuzo ya mchezaji mdogo wa mwaka,
Pep Guardiola amekuwa akimtumia kwenye michezo mbalimbali katika kikosi cha Manchester city
Ndani ya mwaka huu alicheza mchezo wake wa kwanza katika jezi ya city .
Katika ngazi ya kitaifa alishinda kombe la Dunia chini ya miaka 17 pamoja na Tuzo ya dhahabu katika mashindano hayo yaliuofanyika India.
Bradley Lowerey ametunikiwa zawadi ya Hellen Rollason 2017 inayotolewa na BBC kwa hisani ya mwandishi wa kituo hiki aliyefariki kwa ugonjwa wa kansa.
Tuzo hii imewakilishwa kwa Gemma na Carl wazazi wake ,Bradley alifariki kwa ugonjwa wa Kansa mwenzi wa sita alikuwa shabiki mkubwa wa Sunderland pamoja na Jerman Defoe.
Mo Farah ametunikiwa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka katika ardhi ya uingereza ya BBC ya 2017 akimpiku mwana masubwi Antony Joshua , ikiwemo mwanasoka Harry Kane wa spurs.
Mwanariadha huyu ameshinda mataji kama medali ya dhahabu ya olimpiki , dhahabu ya dunia pamoja na dhahabu ya ulaya katika mashindao ya riadha .
makala na Prosper Bartholomew.
simu:/+255716243875.
barua pepe(EMAIL) : Barth prospers gmail.com
Maoni