SABABU YA BARCELONA KUKATAA KUWA WENYEJI WA REAL MADRID KATIKA MCHEZO UJAO HII HAPA

Nmesafiri toka hapa Tanzania mpaka Barcelona kufuatilia kwa nini Klabu hii ya Catalina ikatae kuwa wenyeji wa Real Madrid katika mchezo ujao wa laliga wa el clasico.

Baada ya klabu ya Real Madrid  kutwaa taji la kombe la Dunia la vilabu juzi jumamosi usiku wanatarajia kuwa wenyeji wa mchezo wa kukata na shoka wa el clasico wiki moja baadaye yaani jumamosi inayokuja.

Jana usiku mkurugenzi wa Barcelona wa ushirikiano na uhusiano na michezo bwana Guillermo Amor aliweka wazi kuwa Barcelona hawatatoa heshima kwa mabigwa hawa watakapokutana  kwa kuwa hawakushiriki mashindano hayo , akisema wanatoa heshima kama watakuwa wanashiriki nao shindano husika ,

Wakidai hawatafanya kama  mwaka 2006 walipotoa heshima kwa klabu ya Sevilla walipotwaa taji la kombe la UEFA .

makala na Prosper Bartholomew
simu:/+255716243875
barua pepe (Email) :barthaprosper@gmail.com

Maoni